Kenya yaendeleza usafiri wa kijani kwa kutumia teknolojia ya magari ya umeme ya China
2024-04-24 09:39:50| CRI

Wataalamu wa teknolojia Jumanne walipongeza teknolojia ya magari ya umeme ya China huku Wakenya wakiendelea kukumbatia njia za kijani za usafiri.

Akiongea kwenye mkutano wa pili wa Kampuni ya Usambazaji Umeme kuhusu magari ya umeme, uliofanyika mjini Nairobi nchini Kenya, katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Petroli Alex Wachira alisema magari ya umeme ya China yameibuka kama njia mbadala ya magari ya jadi yanayotumia mafuta. Amezipongeza kampuni zote za China zinazoendesha shughuli za kuunganisha magari nchini Kenya kwa sababu zimechukua jukumu katika kuongeza matumizi ya magari ya umeme nchini humo.

Mkutano huo wa siku mbili umewaleta pamoja zaidi ya wajumbe 200, wakiwemo maafisa wa serikali, wafadhili, na wataalam wa magari ya umeme kutoka kote duniani, ili kuangalia suluhu za kiubunifu na za kimageuzi za kuondoa kaboni katika sekta ya uchukuzi.