Uongozi wa mkoa wa Geita nchini Tanzania watoa tahadhari juu ya ugonjwa wa Kipindupindu
2024-04-24 10:45:29| cri

Uongozi wa Mkoa wa Geita nchini Tanzania umewataka wananchi mkoani humo hususan mjini Geita kuchukua tahadhari na kuzingatia usafi kutokana na ugonjwa wa Kipindipindu.

Akizungumza katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwatulole, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Omar Sukari amesema kuna wagonjwa ambao wamegundulika kuwa na kipindupindu katika mji huo, na kutoa tahadhari hiyo mapema ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.

Hivi karibuni, watoto wawili wa familia moja walifariki kutokana na ugonjwa wa Kipindupindu katika kata ya Nyankumbu mjini Geita, huku wanafamilia wengine wakiendelea kupata matibabu hospitali.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amewataka wananchi kuchukua tahadhari zilizotolewa na idara ya afya ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.