Xi aongoza kongamano la kukuza maendeleo ya eneo la magharibi la China katika zama mpya
2024-04-24 09:38:15| CRI

Rais Xi Jinping wa China Jumanne alisisitiza kuongezwa juhudi za kuanzisha hatua mpya ya maendeleo ya eneo la magharibi la China litakalokuwa na uhifadhi wa mazingira ulioratibiwa vyema, uwazi zaidi na maendeleo yenye sifa bora na ya hali ya juu.

Xi, aliyasema hayo alipokuwa akiongoza kongamano la kukuza maendeleo ya eneo la magharibi mwa China katika zama mpya, ambapo alitoa wito wa kuchukuliwa hatua ili kuandika ukurasa mpya wa maendeleo ya eneo la magharibi.

Alibainisha kuwa eneo la magharibi la China limeshuhudia mafanikio makubwa katika uhifadhi na urejeshaji wa mazingira katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, lakini maendeleo ya eneo hilo bado yanakabiliwa na matatizo na changamoto.

Amesema kuendeleza viwanda ambavyo vinaonyesha nguvu za eneo hilo kunapaswa kuwa lengo kuu, na kwamba juhudi zinahitajika ili kutumia mbinu mahususi ya eneo hilo katika kuendeleza viwanda vinavyoibukia na kuharakisha mageuzi ya viwanda katika eneo la magharibi.