Tamasha la nne la filamu na picha la CMG lafanyika
2024-04-24 10:38:17| cri

Siku ya Lugha ya Kichina, ambayo pia ni tamasha la nne la filamu na picha la Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) lililoandaliwa na CMG pamoja na Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva na ujumbe wa China katika Ofisi hiyo, limefanyika jana huko Geneva kwa mafanikio.

Mkuu wa CMG Shen Haixiong amesema kauli mbiu ya tamasha la mwaka huu ni Ujana, na amewaalika vijana wanaopenda utamaduni wa China duniani kujenga daraja la mawasiliano ya utamaduni, na kutembelea nchini China ili kujionea nchi hiyo katika zama mpya.