UM yatahadharisha athari ya haki za binadamu kwenye sheria ya kuwahifadhi wahamiaji Rwanda iliyopitishwa na Uingereza
2024-04-24 09:35:44| CRI

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulia mambo ya wakimbizi Filippo Grandi na Kamishna Mkuu anayeshughulikia mambo ya haki za binadamu Volker Turk wametahadharisha juu ya Muswada wa Usalama wa wanaotafuta hifadhi na wahamiaji nchini Rwanda, uliopitishwa na Uingereza wiki hii, wakisisitiza athari mbaya juu ya haki za binadamu na ulinzi wa wakimbizi.

Grandi na Turk Jumanne waliitaka serikali ya Uingereza ifikirie upya mpango wake wa kuwahamishia nchini Rwanda wale wanaotafuta hifadhi. Viongozi wa UM badala yake wameitaka Uingereza ichukue hatua za kiutendaji katika kutatua suala la uingiaji usio wa kawaida wa wakimbizi na wahamiaji chini ya msingi wa ushirikiano wa kimataifa na kuheshimu sheria ya haki za binadamu ya kimataifa.