Sudan Kusini yasema haijazuia malori ya misaada ya kibinadamu na mafuta
2024-04-24 23:33:40| cri

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema, wakati Umoja huo unakubali uhakikisho uliotolewa na Sudan Kusini kwamba haizuii malori yaliyobeba misaada ya kibinadamu, lakini malori hayo bado hayajaanza safari zake.

Amesema bado wana wasiwasi kuwa malori ya mafuta bado yanazuiwa katika bohari mbalimbali na mpakani, na hivyo kushindwa kutoa msaada kwa jamii zenye mahitaji nchini Sudan Kusini.

Dujarric amesema, wafanyakazi wa kibinadamu nchini humo wameripoti kuwa, hali kwa sasa ni mbaya huku hifadhi ya mafuta ikikaribia kumalizika. Ameongeza kuwa, mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, Nicholas Haysom ameripoti kuwa hatua za dharura zinahitajika ili malori hayo yaweze kupeleka mahitaji ya kibinadamu.