FAO yakuza kifaa cha ufuatiliaji na tathmini ili kukusanya taarifa za migogoro na mabadiliko ya tabianchi barani Afrika
2024-04-25 10:12:09| CRI

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Jumatano lilisema linakuza kifaa cha ufuatiliaji na tathmini ili kukusanya taarifa za migogoro na mabadiliko ya tabianchi katika nchi za Afrika kusini mwa Sahara.

Mchumi wa ngazi ya juu wa FAO Luca Russo alisema nchi za Afrika kusini mwa Sahara zinaathiriwa vibaya na mabadiliko ya tabianchi na migogoro, changamoto ambazo zinaathiri vibaya usalama wa chakula na kuharibu maisha ya mamilioni ya watu wa huko.

Ofisa huyu aliongeza kuwa kifaa hicho kitasaidia kutambua vitendo vya ufanisi na kuhimiza mazingira ya ushirikiano, ili kupeana uzoefu na ujuzi juu ya mikakati thabiti.