China yatoa wito wa kuungwa mkono kwa eneo la Maziwa Makuu la Afrika
2024-04-25 10:17:26| CRI

Mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Fu Cong Jumatano alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia kukuza amani, usalama na maendeleo katika eneo la Maziwa Makuu la Afrika.

Balozi Fu amesema kwenye Mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu Eneo la Maziwa Makuu kuwa licha ya juhudi za nchi za kikanda, hali tete ya usalama, ghasia zinazoongezeka, pamoja na hali mbaya ya kibinadamu katika eneo hilo zinatia wasiwasi sana. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla wanapaswa kutoa kipaumbele na kuwekeza zaidi katika eneo hilo na kutoa msaada zaidi.

Balozi Fu amesisitiza kwamba ni lazima uhasama upunguzwe na kusitishwa mara moja. Pia China inawapongeza viongozi wa Kenya, Angola, na Sudan Kusini kwa usimamizi wao mzuri. Hata hivyo, machafuko yanayoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yataondoa imani ya wahusika katika kuendeleza mchakato wa amani na kuhatarisha matokeo yaliyopatikana kwa bidii.