Utoaji mkubwa wa chanjo waokoa maisha ya watu milioni 50 barani Afrika
2024-04-25 10:43:56| cri

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema, utoaji wa chanjo inayolenga watoto barani Afrika unakadiriwa kuokoa maisha ya watu milioni 51.2 katika bara hilo katika miongo mitano iliyopita.

Mkurugenzi wa Shirika hilo kanda ya Afrika, Matshidiso Moeti amesema, mamilioni ya watu wako hai hii leo na wana afya njema kutokana na ulinzi unaotolewa na chanjo hizo. Amesisitiza kuwa nchi za Afrika zinapaswa kudumisha na kuongeza utoaji wa chanjo ili kuondokana na magonjwa ya kuambukiza ambayo yanaongoza kwa vifo vya watoto katika bara hilo.

Amesema nchi nyingi za Afrika zinatoa chanjo kwa magonjwa 13 yanayozuilika, ikiwa ni ongezeko kutoka magonjwa 6 ya hapo awali, na hii inatokana na uungaji mkono kutoka taasisi mbalimbali za kimataifa.