Zambia yajitahidi kumaliza ugonjwa wa Malaria kwa maada wa China
2024-04-25 10:43:25| cri

Kaimu mkurugenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Kuondokana na Malaria nchini Zambia, Sampa Chitambala-Otiono amesema, nchi hiyo inajitahidi kuiga uzoefu wa mafanikio ya China katika kuondokana na ugonjwa wa malaria ili kuongeza kasi yake katika kukabiliana na ugonjwa huo.

Bi. Sampa amesisitiza umuhimu wa kujifunza kutoka uzoefu wa China wakati Zambia ikijitahidi kuondokana na malaria itakapofika mwaka 2030, na kuongeza kuwa ingawa hali ya nchi hizo mbili ni tofauti, lakini kuna mambo ambayo wanaweza kujifunza kutoka China ili kuongeza kasi ya kuondokana na malaria.

Pia Bi. Sampa ameishukuru China kwa kuiunga mkono katika mapambano dhidi ya malaria kwa miaka mingi, na kusema China imetoa uungaji mkono wa kutosha ikiwemo kutoa magari kwa ajili ya mradi wa malaria, vifaa vya maabara na pia kutoa program za mafunzo.