Maktaba ya kona ya China yazinduliwa katika kituo cha mafunzo cha Kenya
2024-04-25 10:15:52| CRI

Chuo cha Serikali ya Kenya ambacho ni kituo kinachomilikiwa na serikali kwa ajili ya mafunzo kwa watumishi wa umma, kimezindua maktaba ya kona ya China siku ya Jumatano, iliyosheheni vitabu vinavyohusu ubinadamu na sayansi kutoka China.

Mpango huu unalenga kuwasaidia maafisa wa nchi hiyo kupata uelewa wa kina juu ya historia ya China, mageuzi ya kiuchumi, juhudi za kufufua upya na falsafa ya kisiasa.

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Serikali ya Kenya, Charles Nyachae, alisema kuwa safari ya China ya kurejesha uchumi wa kijamii inatoa msukumo kwa wananchi wa Kenya, na kuonesha umuhimu wa kuelewa maendeleo ya teknolojia, utulivu na utawala wa China.

Maafisa wakuu akiwemo Balozi wa China nchini Kenya Zhou Pingjian walishiriki kwenye uzinduzi wa maktaba ya kona ya China, wakisisitiza umuhimu wa mpango huu katika kuimarisha uhusiano kati ya Kenya na China.