Madai ya Marekani kuhusu “uzalishaji wa kupita kiasi” wa bidhaa za nishati mpya za China ni hatua ya kujilinda kibiashara
2024-04-25 10:35:57| cri

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameanza ziara nchini China jana Aprili 24, na kabla ya ziara hiyo, Marekani ilitangaza kuwa ofisa huyu ataeleza ufuatiliaji wake kuhusu suala la “uzalishaji wa kupita kiasi”wa bidhaa za nishati mpya za China.

Kuhusisha uuzaji wa bidhaa nje ya nchi na kile wanachokiita “uzalishaji wa kupita kiasi”, hakuendani na kanuni za kichumi, na pia ni kinyume na mwelekeo wa utandawazi. Kwa mujibu wa makadirio ya Shirika la Nishati la Kimataifa, ili kutimiza malengo ya uwiano kati ya uzalishaji na unyonyaji wa hewa ukaa (Carbon neutrality), ifikapo mwaka 2030, mahitaji ya magari yanayotumia nishati mpya duniani yatafikia milioni 45. Kwa hivyo, uzalishaji wa leo bado hauwezi kukidhi mahitaji yajayo katika soko la kimataifa, haswa katika nchi zinazoendelea.

Faida linganishi za bidhaa za nishati mpya zilizozalishwa China hazitokani na ruzuku za serikali, na bali zinatokana na uvumbuzi wa kampuni, minyororo kamili ya uzalishaji na ugavi, soko kubwa na akiba kubwa ya raslimali watu.  Ni vema Marekani ijitahidi kupanua faida linganishi za bidhaa zake, badala ya kuzishutumu bidhaa za China kuwa “zinaharibu soko la kimataifa”.

Kwa mtazamo wa kisiasa, uchaguzi mkuu wa Marekani utafanyika mwaka huu, kiongozi wa nchi hiyo hivi karibuni alipotembelea jimbo la Michigan ambalo sekta ya magari ni nguzo yake kuu, aliahidi kuchukua hatua dhidi ya sekta ya magari ya umeme ya China. Kwa hivyo, nadharia ya “uzalishaji wa kupita kiasi”ya Marekani ni kisingizio cha sera ya kujilinda kibiashara, na bali pia ni nyenzo ya kukusanya kura katika uchaguzi ujao.