Naibu Waziri Mkuu wa China Bw. Ding Xuexiang atoa hotuba kwenye ufunguzi wa baraza la Zhongguancun
2024-04-25 23:42:36| cri

Mkutano wa mwaka 2024 wa baraza la Zhongguancun umefunguliwa tarehe 25 hapa Beijing. Mjumbe wa kudumu wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisiti cha China CPC ambaye pia ni naibu waziri mkuu wa China Ding Xuexiang amehudhuria na kutoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano huo.

Bw. Ding Xuexiang amesisitiza kuwa uvumbuzi ni nguvu ya kwanza ya kuhimiza maendeleo. Rais Xi Jinping wa China amesema kuendeleza “Nguvu mpya ya Uzalishaji”ni matakwa na kazi muhimu ya kuhimiza maendeleo ya hali ya juu, hivyo tunahitaji kutoa kipaumbele uvumbuzi.

Bw. Ding Xuexiang pia amesema China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa, kutekeleza ushirikiano wa kimataifa katika sekta ya sayansi na teknolojia kwa wazo la ufunguaji, haki na usawa bila upuuzi, na kujenga umoja wa sayansi na teknolojia duniani kwa pamoja.