China yaahidi kuunga mkono maendeleo ya Zimbabwe yanayochochewa na uvumbuzi
2024-04-26 10:35:02| cri

Balozi wa China nchini Zimbabwe Zhou Ding amesema, China imeahidi kuunga mkono maendeleo ya Zimbabwe yanayochochewa na uvumbuzi.

Akizungumza katika mkutano wa Kimataifa wa Biashara kando ya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Zimbabwe (ZITF), Balozi Zhou amesema, ikiwa chanzo kikuu cha uwekezaji nchini Zimbabwe, China inachukua nafasi muhimu katika kusukuma mbele maendeleo ya uchumi na jamii ya Zimbabwe, hatua iliyoweka msingi wa maendeleo yanayochochewa na uvumbuzi nchini humo.

Naye makamu wa rais wa Zimbabwe Constanino Chiwenga amesema, maendeleo yanayotokana na uvumbuzi ni injini inayoweza kusukuma mbele uchumi wa nchi hiyo. Amesema wakati michakato mipya ya kiviwanda na teknolojia mpya zinapoibuka, mageuzi ya kibiashara pia yanatokea katika ngazi ya kimataifa, na kuongeza kuwa, uvumbuzi unawezesha Zimbabwe kuwa na uhusiano imara zaidi wa kibiashara na kuanzisha masoko na fursa mpya za kibiashara duniani.