Kenya yaimarisha maandalizi ya dharura huku mafuriko yakisababisha vifo vya watu zaidi ya 50
2024-04-26 10:00:57| CRI

Kenya Alhamisi ilisema imeimarisha hatua za dharura ili kukabiliana na mafuriko kwenye sehemu mbalimbali nchini humo yanayosababishwa na mvua kubwa inayoendelea.

Naibu rais wa Kenya Rigathi Gachagua amesema serikali imeunda timu ya kitaifa yenye idara nyingi ya kukabiliana na mafuriko na kituo cha kukabiliana na majanga, ili kusaidia kuzuia mafuriko yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 50.

Gachagua alitangaza hatua hizo baada ya mkutano ulioendeshwa na rais William Ruto wa Kenya huko Nairobi, akiwahakikishia watu kuwa serikali inafahamu hali ya mafuriko na imeimarisha kukabiliana na janga hilo. Gachagua amesema watu wote waliokosa makazi nchini humo watatafutiwa haraka makazi mbadala.