Kupinga Adhabu ya viboko kwa watoto
2024-04-27 09:44:00| CRI

Katika miaka ya karibuni, ama siku za karibuni, kumekuwa na matukio mengi ya watoto kuchapwa viboko na kuwasababishia maumivu makali mwili ama hata vifo. hatukatai kwamba mtoto ni lazima apewe adhabu, lakini tunapowaadhibu watoto, kuna mambo ambayo hatuna budi kuyazingatia, ikiwemo umri, aina ya kosa, na kama adhabu tunayotoa inaendana na kosa husika. 

niliwahi kusoma gazeti moja la nchini Kenya ambako mwanafunzi alifariki baada ya kupewa adhabu ya kulima tena mchana wakati wa jua kali. mwalimu aliyetoa adhabu hiyo hakuzingatia afya ya mwanafunzi bali alilazimisha adhabu hiyo ifanyike kwa wakati huo. Sasa, ikiwa Aprili 30 ni siku ya kupinga adhabu ya viboko kwa watoto, leo hii katika kipindi hiki cha Ukumbi wa Wanawake tutazungumzia zaidi kuhusu adhabu hiyo.