Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Tanzania wapongeza maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano kati ya nchi zao
2024-04-28 09:54:52| cri

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi na mwenzake wa Tanzania Bw. January Makamba tarehe 26 Aprili wamepeana salamu za pongezi za maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano kati ya nchi zao. Bw. Wang Yi amesema, tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi, China na Tanzania zimekuwa marafiki na wenzi wazuri ambao wanaheshimiana, kuaminiana na kujiendeleza kwa pamoja. Ameongeza kuwa anapenda kushirikiana na mwenzake wa Tanzania, kuimarisha mazungumzo na ushirkiano kati ya wizara za mambo ya nje za China na Tanzania, kuhimiza kutekeleza maoni makuu ya pamoja yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili, na kutoa mchango zaidi kwa ajili ya maendeleo endelevu ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Tanzania. Bw. Makamba amesema urafiki wa kindugu kati ya Tanzania na China una msingi imara tangu siku zilizopita, na utaendelea kuimarishwa katika miaka 60 ijayo. Pia amesema Tanzania inapenda kushirikiana na China kukabiliana na changamoto na kutimiza malengo ya pamoja.