Watu 90 wafariki kutokana na mafuriko nchini Kenya
2024-04-29 08:52:59| CRI

Mamlaka nchini Kenya zimeonya kuhusu ongezeko la vifo na uharibifu wa mali baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko nchini humo.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi nchini himo, watu 90 wamefariki huku kukiwa na wasiwasi kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka kutokana na miili mengi kusombwa na maji. Pia Polisi wamethibitisha kuwa, wamepata miili 11 kutoka maeneo mbalimbali jumamosi usiku wakati mvua kubwa ikiendelea kunyesha nchini humo na kusababisha vifo vya watu kadhaa waliokuwa wakijaribu kuvuka mito iliyokuwa imefurika.

Makamu wa rais wa Kenya Rigathi Gachagua amesema ijumaa iliyopita, kwamba serikali imechukua hatua kadhaa ikiwemo kutenga dola za kimarekani milioni 30 kwa ajili ya kushughulikia kwa haraka madhara yanayosababishwa na mvua hizo.

Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Kenya Japhet Koome amesema wamepeleka maofisa zaidi katika barabara mbalimbali kusaidia kutoa maelekezo kwa maderava wa magari na watumiaji wengine wa barabara.