Maonyesho ya “China Image” yazinduliwa Hungary
2024-04-29 22:30:28| cri

Maonyesho ya “China Image” yamezinduliwa Budapest, nchini Hungary kwa kuandaliwa pamoja na Shirika Kuu la Radio na Televisheni ya China CMG na televisheni ya ATV ya Hungary.

Kazi bora za filamu na televisheni zaidi ya kumi zitatangazwa kwenye vyombo vya habari vya Hungary, zikiwasilisha nguvu ya uhai ya China katika enzi mpya kwa watazamaji wa Hungary, na kusimulia hadithi za mawasiliano ya kirafiki kati ya watu wa China na Hungary, na kuonyesha maelewano na ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili.