Xi kufanya ziara Ufaransa, Serbia na Hungary kuanzia tarehe 5 hadi 11, Mei
2024-04-29 22:31:15| cri

Rais Xi Jinping wa China atafanya ziara za kiserikali nchini Ufaransa, Serbia na Hungary kuanzia tarehe 5 hadi 11, Mei kwa mwaliko wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Rais wa Serbia Aleksandar Vučić na Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orbán.