Afisa wa FAO aonya kuhusu janga la njaa ambalo halijawahi kutokea nchini Sudan
2024-04-29 10:20:46| cri

Vita inayoendelea nchini Sudan iliyoanza Aprili 15, 2023 imedumu kwa zaidi ya mwaka mmoja, na kusababisha maafa makubwa ya kibinadamu kwa nchi hiyo, ikiwemo ukosefu wa usalama wa chakula.

Mkurugenzi wa Ofisi ya Operesheni za Dharura na Ustahimilivu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Bw. Rein Paulsen hivi karibuni amesema, karibu watu milioni 18 nchini Sudan wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, na kwamba kama hatua za haraka hazitachukuliwa, njaa isiyo na kifani inaweza kuenea nchini humo.

Ameongeza kuwa, zaidi ya Wasudan milioni 2 waliokimbilia nchi jirani kama Chad na Sudan Kusini, wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, maji ya kunywa na vifaa vya matibabu na afya.