Msomi wa Côte d’Ivoire:Njia ya China kuelekea kuwa nchi ya kisasa yatoa mfano wa kuigwa kwa Afrika
2024-04-30 10:38:30| CRI

Msomi wa Côte d’Ivoire Prof. Bamba Abdoulaye amesema hivi karibuni kuwa,  njia ya China kuelekea kuwa nchi ya kisasa si kama tu ina sifa za pamoja za njia za nchi mbalimbali kujenga mambo ya kisasa, bali pia ina umaalum wa kipekee unaoendana na hali yake halisi. Njia hiyo ya China ya kujijenga kuwa nchi ya kisasa imetoa mfano wa kuigwa kwa nchi za Afrika.

Prof. Bamba Abdoulaye wa historia ya mahusiano ya kimataifa katika Chuo Kikuu cha Félix Houphouët-Boigny nchini Côte d’Ivoire, amesema nchi za Afrika zinaweza kujifunza kutokana na uzoefu wa China katika kujijenga kuwa nchi ya kisasa, kuweka mipango ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii inayofaa hali zao zenyewe, na kuwaongoza wananchi waondokane na umaskini. Prof. Abdoulaye amesema, China inaweka mkazo katika kulinda maslahi ya wananchi wote, na wala sio maslahi ya baadhi ya makundi madogo madogo, mtazamo huu wa kisiasa unastahili kuigwa na nchi za Afrika. Anaona, Waafrika kutoka nyanja zote za maisha barani Afrika wanapaswa kuja China kujionea wenyewe, ili kuimarisha ufahamu wao kuhusu njia ya China ya kuelekea kuwa ya kisasa, na hivyo kuwasaidia washikilie vyema mustakbali na hatma yao wenyewe.

Prof. Bamba Abdoulaye  ameongeza kuwa, njia ya China ya kujijenga kuwa nchi ya kisasa ni njia ya kujiendeleza kwa amani. China siku zote inafuata sera ya diplomasia ya amani na ya kujitegemea, na kuunga mkono dunia iwe na usawa, utaratibu na ncha nyingi. China inaitilia maanani Afrika, inaiheshimu Afrika, na inaiunga mkono Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni, hasa chini ya msukumo wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”(BRI), China imeisaidia Afrika kujenga barabara na madaraja, na kuiletea teknolojia, ushirikiano kati ya pande hizo mbili unaendelea kuimarika. Prof. Abdoulaye anaona, China ni rafiki wa dhati kwa Afrika, na Afrika na China zinapaswa kuimarisha mawasiliano na kufunzana.