China yashtushwa na ripoti ya kugunduliwa kwa makaburi ya halaiki katika Ukanda wa Gaza
2024-04-30 09:14:10| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lin Jian amesema, China imeshtushwa na ripoti kuhusu kugunduliwa kwa makaburi mawili ya halaiki katika Ukanda wa Gaza.

Kulingana na ripoti hiyo, mamia ya miili ilipatikana ikiwa imezikwa katika Hospitali ya Nasser na Hospitali ya Al-Shifa katika Ukanda wa Gaza.

Bw. Lin Jian amesisitiza kwamba, ni lazima kuhimiza kusimamisha vita haraka iwezekanavyo, na nchi husika hazipaswi kupuuza wito wa haki unaotolewa na jumuiya ya kimataifa. Amesema pande hizo zinapaswa kutekeleza mara moja maazimio husika ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kufikia makubaliano yasiyo na masharti na ya kudumu ya kusimamisha vita, na kuchukua hatua madhubuti kukomesha kabisa janga hili kubwa la kibinadamu la karne ya 21.