CMG yatangaza vipindi vya chakula na utamaduni kati ya China na Ufaransa
2024-04-30 19:16:06| CRI

Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) likishirikiana na Ubalozi wa Ufaransa nchini China limetangaza vipindi vya chakula na utamaduni kati ya China na Ufaransa vinavyoitwa “Wakati wa kung’ara: Mashindano ya upishi kati ya mabingwa wa China na Ufaransa”.

Mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong, balozi wa Ufaransa nchini China Bertrand Lortholary, Mkuu wa Makumbusho ya Sanaa ya Taifa la China Bw. Wu Weishan walihutubia hafla hiyo na kuzindua kwa pamoja vipindi hivyo.

Katika hafla hiyo Bw. Shen Haixiong amesema, vipindi hivyo vitaonesha mila na utamaduni wa China na Ufaransa, na kukuza maingiliano kati ya watu wa nchi hizo mbili. Ameongeza kuwa, CMG ingependa kujifunza kutoka kwa marafiki wa sekta mbalimbali nchini Ufaransa, na kuelekea kwa pamoja mustakabali mzuri.