Chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-17 charudi duniani na kutua kwa mafanikio
2024-05-01 08:44:43| CRI

Chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-17 kimerudi duniani na kutua kwa mafanikio tarehe 30 Aprili.

Madaktari wamethibitisha kuwa wanaanga watatu waliokuwa kwenye chombo hicho wako katika hali nzuri ya kiafya, na kuonesha kuwa jukumu la chombo cha Shenzhou-17 limepata mafanikio mazuri.

Chombo cha Shenzhou-17 kilichorushwa katika anga za juu tarehe 26 Oktoba mwaka 2023 kutoka Kituo cha Kurushia Satelaiti cha Jiuquan, kiliungana na moduli ya Tianhe katika Kituo cha Anga ya Juu cha China. Walipokuwa katika anga ya juu, wanaanga watatu walisafiri kwa siku 187, na kutembea nje ya chombo hicho mara mbili na kufanya kazi mbalimbali za uundaji, marekebisho na utengenezaji wa vifaa vya kituo hicho, na majaribio mengi ya kisayansi.