Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko nchini Kenya yafikia 169
2024-05-01 08:46:32| CRI

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Kenya imefikia 169.

Msemaji wa serikali ya Kenya Isaac Mwaura amethibitish idadi hiyo ya vifo jumatatu jioni, na kusema serikali imeongeza operesheni za uokoaji ili kuwapata watu walioripotiwa kuwa hawajulikani walipo.

Amesema timu ya dharura iliyoundwa na taasisi mbalimbali kukabiliana na athari za mafuriko inatekeleza hatua kadhaa ili kuwasaidia Wakenya kukabiliana na athari za mafuriko, ikiwemo kugawa chakula, maji safi ya kunywa, mahitaji ya kiafya na juhudi za uokoaji.

Mafuriko hayo yameongeza mgogoro wa kibinadamu nchini Kenya ikiwa ni baada ya mafuriko yaliyosababishwa na mvua za El Nino mwishoni mwa mwaka jana ambapo watu 178 walifariki, 242 kujeruhiwa na wengine wengi kukosa makazi.