Umoja wa Afrika watoa wito wa mfumo mpya wa kifedha ili kukabiliana na mahitaji ya bara hilo
2024-05-01 08:45:59| CRI

Umoja wa Afrika (AU) umetoa wito wa kuanzishwa kwa mfumo wa kifedha wa maendeleo utakaojibu mahitaji ya bara hilo, ikiwemo kukabiliana na migogoro kama mabadiliko ya tabianchi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye pia ni rais wa Mauritania, Mohamed Cheikh Ghazouani katika taarifa yake baada ya Mkutano wa Shirikisho la Kimataifa la Maendeleo ulioandaliwa na Benki ya Dunia (IDA 21) na kufanyika mjini Nairobi, Kenya. Amesema mfumo wa fedha uliopo sasa hauziwezeshi nchi nyingi za Afrika kukabiliana na malengo yao na kuongeza kuwa, inahitajika kuansisha mzunguko wa uelewa na uwekezaji katika mtaji wa watu ili kuweza kuwa na ushindani duniani.

Rais Ghazouani amewataka wenza wa maendeleo na wafadhili wa IDA kuchangia fedha zinazohitajika ili Afrika iweze kushinda changamoto zake na kutimiza maendeleo endelevu.