Wajumbe wa makundi ya Fatah na Hamas wakutana nchini China
2024-05-01 08:46:50| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Lin Jian amesema, wawakilishi wa makundi ya Fatah na Hamas ya nchini Palestina hivi karibuni walikutana hapa Beijing kwa mashauriano ya kina na ya wazi juu ya kukuza maridhiano ya ndani ya Palestina.

Bw. Lin amesema, pande hizo mbili zimeeleza kikamilifu nia yao ya kisiasa ya kufikia maridhiano kwa njia ya mazungumzo na mashauriano, na kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali muhimu na kupata maendeleo chanya. Pia pande hizo zimekubaliana kwa kauli moja kuendeleza mchakato huo wa mazungumzo na kujitahidi kufikiwa mapema umoja na mshikamano wa Wapalestina.

Bw. Lin pia amesema, pande zote mbili zimeshukuru uungaji mkono thabiti wa China katika suala la haki ya watu wa Palestina na kurejesha haki zao halali za kitaifa, na kwa juhudi za China katika kuhimiza uimarishaji wa umoja wa ndani wa Palestina .