Kundi la Hamas lasema litasitisha mazungumzo ya kusimamisha mapigano katika Ukanda wa Gaza kama Israel itashambulia Rafah
2024-05-02 08:18:17| cri

Kundi la Hamas la Palestina limesema mazungumzo ya kusimamisha mapigano na Israel yatasitishwa iwapo Israel itaushambulia mji wa Rafah ulioko kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Afisa mwandamizi wa kundi la Hamas Bw. Osama Hamdan ameishutumu Israel kwa kutaka kuzitisha pande zote kwa madai ya kushambulia Rafah, na kusisitiza kwamba, kundi lake bado lina nguvu za kutetea watu wake.

Habari zinasema, Waziri Mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu amesema Israel itaingia Rafah na kuwaondoa wapiganaji wa kundi la Hamas walioko huko bila kujali kama itafikia makubaliano na Hamas ama la.