Uganda yaitaka Uingereza kuacha kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi hiyo
2024-05-02 08:20:08| CRI

Uganda imeitaka Uingereza kuacha kuingilia kati mambo ya ndani ya kisiasa ya nchi hiyo baada ya Uingereza kutangaza vikwazo dhidi ya maofisa watatu wa ngazi ya juu wa Uganda kwa madai ya ufisadi.

Taarifa iliyotolewa na Bunge la Uganda imeitaka Uingereza kuheshimu mamlaka ya nchi hiyo, na kuepuka jaribu la kuingilia kati siasa za ndani za nchi hiyo, ikiwemo kulazimisha wafanya maamuzi kufuata mifumo yao ya maadili, hususan katika suala la mapenzi ya jinsia moja.

Serikali ya Uingereza jumanne wiki hii ilitangaza kuwa imewawekea vikwazo Spika wa Bunge la Uganda Anita Among na wabunge wengine wawili, Goretti Kitutu na Agnes Nandutu kwa tuhuma za ufisadi.