MONUSCO yaondoka kutoka mkoa wa Kivu Kusini nchini DRC
2024-05-02 08:18:44| CRI

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema, Tume ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) MONUSCO imemaliza operesheni yake katika Mkoa wa Kivu Kusini nchini humo.

Amesema hatua hiyo inafuatia Azimio No.2717 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lililopitishwa mwezi Desemba mwaka jana, ambapo Baraza hilo limeidhinisha MONUSCO kujiondoa kutoka Kivu Kusini mwishoni mwa mwezi Aprili.

Bw. Dujarric pia amesema kutokana na hatua hiyo, majukumu ya tume hiyo ikiwa ni pamoja na kulinda raia, yamekamilika katika mkoa wa Kivu Kusini, na kwamba mashirika ya Umoja wa Mataifa, ufadhili wa fedha na miradi itaendelea kubaki mkoani humo ili kutoa msaada kuendana na majukumu yao yenyewe.