Watu 50 wafariki kutokana na mvua kubwa nchini Rwanda katika miezi miwili
2024-05-03 08:44:05| CRI


Waziri wa Masuala ya Dharura nchini Rwanda, Bw. Albert Murasira amesema, athari zilizotokana na mvua kubwa ikiwemo maporomoko ya udongo na radi, zimesababisha vifo vya watu 49 na wengine 79 kujeruhiwa nchini humo katika miezi miwili iliyopita.

Bw. Murasira amesema, watu 12 wamefariki kwa kupigwa na radi huku wengine wakifariki kwa kuangukiwa na nyumba zao mbovu.

Ameongeza kuwa serikali imewahamisha wakazi karibu elfu 5 kutoka maeneo yenye hatari kubwa hadi maeneo salama kote nchini.

Maafa hayo pia yameharibu miundombinu, ikiwemo nyumba, madaraja, majengo ya shule, mitandao ya barabara pamoja na mashamba.