Rais William Ruto wa Kenya jana Alhamisi alitangaza kumpandisha cheo Luteni Jenerali Charles Muriu Kahariri kuwa Jenerali, na kumteua kuwa mkuu mpya wa jeshi la ulinzi la nchi hiyo, kufuatia kifo cha Jenerali Francis Ogolla.
Jenerali Kahariri ambaye alijiunga na jeshi la ulinzi la Kenya mwezi Aprili mwaka 1987, alikuwa makamu mkuu wa jeshi hilo.
Siku hiyo hiyo, kamanda wa jeshi la anga la Kenya Meja Jenerali John Omenda alipandishwa cheo kuwa Luteni Jenerali, na kuteuliwa kuwa Makamu mkuu wa jeshi la ulinzi la Kenya.