Kenya yakabiliwa na hasara kubwa kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua
2024-05-03 10:09:08| CRI

Kenya inakabiliwa na hasara kubwa kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayofikia milimita 200 kwa siku, ambapo watu wasiopungua 188 wamefariki na makumi ya maelfu ya watu kupoteza makazi yao.

Mvua hizo zimeathiri sekta mbalimbali kote nchini. Mji mkuu Nairobi unaathiriwa zaidi, ambapo biashara nyingi zilizokuwa nzuri sasa zimeharibika kutokana na mafuriko.

Utabiri wa hali ya hewa unaonyesha kuwa, mvua hizo zitaendelea mpaka Julai, huku sehemu nyingi nchini humo zina uwezekano wa kuwa na kiwango cha wastani na juu ya wastani cha mvua.