UNGA latangaza mwaka 2026 kuwa mwaka wa kimataifa wa wakulima wanawake
2024-05-03 08:49:55| cri

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) jana lilipitisha azimio la kuutangaza mwaka 2026 kuwa Mwaka wa Kimataifa wa Wakulima Wanamke.

Azimio hilo linakaribisha ufuatiliaji wa dunia nzima wa Mwaka wa Kimataifa, kupitia shughuli zinazolenga kuongeza uelewa na kuelekeza umakini wa kisera kwa vikwazo na changamoto zinazowakabili wakulima wanawake katika mifumo ya kilimo, pamoja na mipango, sera na hatua zinazoweza kuchukuliwa kushughulikia masuala hayo na kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake wote katika sekta ya kilimo.

Baraza hilo limelitaka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na mashirika mengine ya Umoja huo nchini Italia kuwezesha utekelezaji wa azimio hilo na kuzingatia Mwaka wa Kimataifa.