Ubalozi wa China nchini Zambia kuandaa kongamano kuhusu maendeleo ya ubora wa juu
2024-05-03 08:22:32| CRI

Ubalozi wa China nchini Zambia kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Zambia, utaandaa kongamano la kujadili fursa za ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Balozi wa China nchini Zambia Du Xiaohui amesema, zaidi ya kampuni 200 za China na Zambia zimejiandikisha kuhudhuria Kongamano la Maendeleo ya Ubora wa Juu kati ya China na Zambia litakalofanyika tarehe 15 mwezi huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenneth Kaunda mjini Lusaka, na kuongeza kuwa, zaidi ya wafanyabiashara 200 kutoka China wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo.

Waziri wa Biashara na Viwanda wa Zambia Chipoka Mulenga amesema, kongamano hilo ni muhimu kwa nchi zote mbili, na kuwataka wafanyabiashara wa Zambia kutumia fursa hiyo kuwasiliana na wenzao wa China.