Kamanda mkuu wa wapiganaji wanaotaka kujitenga nchini Cameroon ni miongoni mwa watu watatu waliouawa
2024-05-06 08:21:57| CRI

Wapiganaji watatu wanaotaka kujitenga nchini Cameroon akiwemo kamanda mkuu, waliuawa wakati vikosi vya serikali viliposhambulia maficho yao siku ya Jumapili katika eneo lisilo na utulivu la watu wanaozungumza Kiingereza Kaskazini Magharibi mwa Cameroon.

Msako huo uliothibitishwa na afisa mmoja wa kijeshi wa eneo hilo ambaye hakutaka kutajwa jina, ulianza alfajiri ya Jumapili katika tarafa ya Ngoketunjia mkoani humo. Miongoni mwa waliouawa ni kamanda mkuu aliyejiita "Jenerali Sagon."

Afisa mmoja katika eneo hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe aliiambia Xinhua kwamba kuuawa kwake ni kikwazo "kikubwa" kwa waasi wanaotaka kujitenga katika eneo hilo.

Mapigano kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wanaotaka kujitenga yameendelea katika maeneo mawili ya Cameroon yanayozungumza Kiingereza ya Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi tangu 2017 wakati watu wanaotaka kujitenga walipojaribu kuanzisha taifa huru katika maeneo haya.