China na Ufaransa zajiandaa kuimarisha uhusiano wakati hali ya kimataifa inashuhudia mabadiliko
2024-05-06 08:37:02| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana Jumapili aliwasili Paris kwa ziara ya kiserikali nchini Ufaransa, ambapo nchi hizi mbili zimejiandaa kuimarisha uhusiano kati yao na kusisitiza ahadi yao ya kuongeza ushirikiano wakati hali ya kimataifa inashuhudia mabadiliko.

Majadiliano na makubaliano kwenye ziara ya tatu ya kiserikali ya Rais Xi nchini Ufaransa, kufuatia ziara zake zilizopita katika mwaka wa 2014 na 2019, yanatarajiwa kuhusisha nyanja nyingi muhimu. Kutoka biashara na uwekezaji hadi uvumbuzi na mawasiliano ya kiutamaduni, ajenda ya ziara hiyo inaakisi uhusiano unaohusisha nyanja zote kati ya China na Ufaransa.

Katika ziara hiyo, viongozi wa nchi hizo mbili pia wanatarajiwa kubadilishana maoni kuhusu masuala ya kikanda na kimataifa wanayoyafuatilia kwa pamoja, na ushirikiano wa pande nyingi.