Serikali ya Kenya kukusanya maji ya mvua ili yatumike wakati wa kiangazi
2024-05-06 21:36:10| cri

Serikali ya Kenya ina mpango wa kukusanya maji ya mvua ili kuyahifadhi kwa matumizi ya siku zijazo.

Katibu wa Idara ya Umwagiliaji Maji Mashambani nchini humo Ephantus Kimotho amesema, hiyo ni njia bora ya kuhifadhi maji ili kuyatumia siku za kiangazi. Amesema tangu mvua kubwa ianze kunyesha, maji mengi yamepotea bure ambayo kama yangekusanywa na kuhifadhiwa kwa matumizi ya siku zijazo, ingekuwa ni faida kubwa katika uzalishaji wa chakula na kwa matumizi mengine.

Bw Kimotho amesema, kupitia mradi huo, wakulima watapata maji mengi ya kumwagilia mashamba yao huku mengine yakisafishwa na kuwa maji safi ya kunywa.