Idadi ya waliofariki kwa mafuriko nchini Kenya yapanda hadi 228, Kimbunga Hidaya chapoteza nguvu baada ya kutua
2024-05-06 08:22:37| CRI

Mamlaka ya Kenya Jumapili ilisema watu tisa zaidi walipoteza maisha yao katika saa 24 zilizopita kutokana na mafuriko makubwa na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa, na kufanya idadi ya vifo kufikia 228.

Hata hivyo Wizara ya Mambo ya Ndani ilifafanua kuwa kimbunga Hidaya katika Bahari ya Hindi kimepoteza nguvu kufuatia kutua katika Kisiwa cha Mafia nchini Tanzania Jumamosi. Wizara hiyo ilisema kutokana na Kimbunga Hidaya marufuku ya shughuli za ufukweni zikiwemo uvuvi, kuogelea na usafiri usio wa lazima ndani ya eneo la maji ya nchi hiyo  yataendelea hadi usiku wa manane wa Mei 6.

Wizara imebainisha kuwa dhoruba ya Kimbunga Hidaya imekamilika na kinatabiriwa kupungua, hata hivyo, mvua kubwa bado  inatazamiwa kunyesha katika eneo la pwani huku kukiwa na upepo mkali na mawimbi makubwa ambayo tayari yameshuhudiwa katika Kaunti ya Kwale.

Takriban watu 227,238 wameathiriwa na mvua hiyo kubwa huku jumla ya shule 1,967 zikiathiriwa na mafuriko.