Hamas kutoa jibu la mwisho kwa pendekezo jipya la usitishwaji vita ndani ya siku mbili
2024-05-06 08:45:26| CRI

Chanzo cha habari cha Palestina kimesema, ujumbe wa Hamas Jumanne utarudi Cairo, mji mkuu wa Misri kutoa jibu la mwisho la kundi hilo kwa pendekezo lililotolewa na Misri kuhusu kusimamisha vita katika Ukanda wa Gaza na kubadilishana wafungwa na Israel.

Kwa mujibu wa Chanzo hicho kisichotaka kutajwa jina, katika mazunguzo ya siku mbili yaliyofanyika huko Cairo, ujumbe wa Hamas ulikutana na maofisa wa usalama wa Misri na kushughulikia masuala yote yanazoweza kuzuia kufikiwa kwa makubaliano ya kusimamisha vita huko Gaza na kubadilishana wafungwa na Israel, na kuthibitisha kwamba makubaliano muhimu yamefikiwa na ujumbe huo na Misri.

Pendekezo lililotolewa na Misri lina hatua tatu, ambazo ni kubadilisha mateka wa Israel kwa wafungwa wa Palestina, kuchukua hatua za lazima ili kutimiza usitishaji vita na kurejesha utulivu wa kudumu.