Mke wa rais wa China atembelea makao makuu ya UNESCO na kukutana na mkuu wa shirika hilo
2024-05-07 09:36:12| CRI

Mke wa rais Xi Jinping wa China Bi. Peng Liyuan, ametembelea makao makuu ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO).

Bi. Peng alipowasili, alikaribishwa na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo Bi. Audrey Azoulay, na baadaye aliambatana na Bi. Peng kwenda kutembelea maonesho ya mafanikio ya miaka kumi ya ushirikiano kati ya China na UNESCO. Bi. Azoulay aliipongeza China kwa kutoa mchango katika kuhimiza maendeleo ya shughuli za elimu ya watoto wa kike na wanawake duniani.

Naye Bi. Peng alielezea kwa ujumla maendeleo mapya yaliyopatikana China katika kuhimiza elimu ya watoto wa kike na wanawake, hasa maendeleo yaliyopatikana katika mradi wa “Spring Bud”. Bi. Peng amesema, katika miaka kumi iliyopita tangu awe balozi maalum wa kuhimiza elimu ya watoto wa kike na wanawake wa UNESCO, ametembelea shule za nchi nyingi, ambapo alifurahia kuona wanawake wengi zaidi wanabadilisha hatma yao kupitia elimu na kuishi maisha yenye furaha.