Uganda yatangaza hatua za kudhibiti ubora wa hewa
2024-05-07 22:05:56| cri

Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira ya nchini Uganda (NEMA) imesema, nchi hiyo imependekeza hatua zinazolenga kudhibiti ubora wa hewa.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Barirega Akankwasah amesema, kuna haja ya kuingilia kati suala hilo kutokana na kwamba nchi hiyo inapoteza watu 31,600 kila mwaka kutokana na magonjwa yanayohusiana na uchafuzi wa hewa. Amesema ili kukabiliana na hali hiyo, kwa mara ya kwanza Uganda imeanzisha vigezo vya kitaifa na kanuni kwa ajili ya usimamizi wa ubora wa hewa.

Ameongeza kuwa, viwanda vyote vinatakiwa kuweka vifaa vya kusimamia ubora wa hewa vinavyojiendesha ambavyo vinapeleka data moja kwa moja kwenye kituo kikuu cha kanzidata.