Wakati Rais Xi Jinping wa China alipofunga safari ya kwenda Belgrade kufanya ziara rasmi nchini Serbia, ametoa makala kwenye Gazeti la Siasa la nchi hiyo.
Kwenye makala yake Rais Xi amesema China iko mbali na Serbia, lakini watu wa nchi hizo mbili siku zote wanashikamana, na bila ya kujali mabadiliko gani yanayotokea duniani, nchi hizo mbili ni marafiki na wenzi wakubwa.
Amesisitiza kuwa mawasiliano ya kirafiki na ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili kwa muda mrefu vimethibitisha kuwa, kukua kwa uhusiano wao kunalingana na mkondo wa historia na maslahi makuu ya watu, na kunahimiza maendeleo ya nchi hizo mbili.
Ameongeza kuwa kwa kupitia ziara hiyo, anapenda kushirikiana na Serbia kuchukua hatua halisi zitakazowanufaisha zaidi wananchi wa nchi hizo mbili, kuhimiza amani na maendeleo duniani, na kusukuma mbele kwa pamoja ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye muskatabali wa pamoja.