Likizo ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yashuhudia mwelekeo mzuri wa ukuaji wa uchumi wa China
2024-05-07 13:43:56| cri

Takwimu rasmi zilizotolewa na serikali ya China zinaonyesha kuwa, wakati wa likizo ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, idadi ya watu wanaosafiri nchini China ilifikia milioni 295, ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.6 kuliko mwaka jana wakati kama huu.

Takwimu hizo pia zimeonyesha kuwa, matumizi ya fedha katika kipindi hicho yalifikia yuan milioni 166.89, sawa na dola za kimarekani milioni 23.15.

Utalii katika sehemu za tarafa umeibuka, huku miji maarufu ikileta miradi mipya ya kitamaduni inayopendwa na watalii, hali ambayo imeonesha kupanda ngazi kwa mahitaji ya matumizi ya wakazi wa China.

Wakati huo huo, baada ya kurejeshwa kwa safari za ndege, utekelezaji wa taratibu zilizorahisishwa za forodha, na ongezeko la idadi ya nchi zinazofuta hitaji la viza na China, usafiri wa watalii wa kigeni nchini China umefufuka kwa kasi. Takwimu zinaonesha kuwa, wakati wa likizo hiyo, watalii wa China wamesafiri katika zaidi ya miji 1,000 duniani, na kuleta ufufukaji wa masoko ya matumizi ya huko. Kati ya nchi hizo, idadi ya watalii katika nchi zinazoondoa hitaji la viza ya utalii na China inaongezeka kwa udhahiri. Kwa mujibu wa Gazeti la Lianhe Zaobao la Singapore, ukataji wa tiketi za ndege za kwenda Singapore kutoka China wakati wa likizo hiyo uliongezeka kwa zaidi ya mara mbili. Baada ya Cuba kutangaza kusamehe viza kwa raia wa China hivi karibuni, utafutaji wa maneno kuhusu hoteli za Cuba na tiketi za usafiri wa ndege kwenda Cuba katika tovuti za utalii nchini China umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 40. Waziri wa Utalii wa Cuba Juan García anaona kuwa hatua hii italeta fursa mpya kwa maendeleo ya utalii wa nchi hiyo na Latin Amerika.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, China imetangaza sera mfululizo za kuhimiza matumizi, Wizara ya Biashara ya China pia imetangaza mwaka huu kuwa “Mwaka wa Kukuza Matumizi”, na kuandaa shughuli mbalimbali zinazohusika, hatua ambazo si kama tu zimekidhi mahitaji tofauti na yenye hali ya juu ya wachina, bali pia inachochea nguvu ya soko la ndani la matumizi la China.

Takwimu mpya zimeonesha kuwa, matumizi katika robo ya kwanza ya mwaka yamechangia asilimia 73.7 ya ukuaji wa uchumi wa China. Wakati China inapoandaa masoko mapya kama vile matumizi ya dijitali, matumizi ya kijani na matumizi ya afya na kuzidi kuhimiza ongezeko la masoko mapya ya matumizi, vilevile itatia nguvu mpya kwa maendeleo ya uchumi wa dunia.