Mamlaka ya Usimamizi wa Masoko ya Mitaji ya Afrika Mashariki (EASRA) zimekubaliana kuanzisha mfumo wa kikanda unaolenga kuboresha upatikanaji wa masoko ya mitaji katika kanda hiyo.
Katika taarifa yake iliyotolewa mjini Nairobi, Kenya, jana, Mwenyekiti wa Mamlaka hiyo Josephine Osiya amesema, mfumo huo utawezesha soko la mitaji kukusanya fedha zinazotumika katika kukabiliana na athari hasi za mabadiliko ya tabianchi. Pia amesema, mfumo huo utatoa vigezo vya kusimamia uendelevu vinavyohusiana na mauzo ya hisa, matumizi ya fedha zinazopatikana, kufanya tathmini na kutoa ripoti.