Wake wa marais wa China na Ufaransa watembelea Jumba la Makumbusho la Orsay
2024-05-07 09:34:26| CRI

Mke wa rais Xi Jinping wa China Bi. Peng Liyuan tarehe 6 mwezi huu alitembelea Jumba la Makumbusho la Orsay akiwa pamoja na mke wa rais Emmanuel Macron wa Ufaransa Bi. Brigitte Macron.

Bi. Peng aliangalia michoro mingi maarufu ya wachoraji nguli, ambapo alisema kuwa watu wa China na Ufaransa wote wanapenda sanaa ya uchoraji na nchi hizo mbili zinatarajiwa kuwasiliana zaidi katika sekta husika ili kuzidisha maelewano kati ya watu wao. Aidha wasanii wa nchi hizo mbili wanatarajiwa kuhimiza mawasiliano na kubuni kazi nyingi zaidi nzuri za sanaa.

Wake hao wa viongozi pia wamezungumza na wanafunzi wa Ufaransa waliotembelea jumba hilo. Wanafunzi hao wameeleza uzoefu wao wa kujifunza Kichina, ambapo Bi. Peng amesema anatarajia kwamba watatembelea nchini China wakipata fursa na kuendeleza urafiki kati ya nchi hizo mbili.