China yapenda kufanya juhudi pamoja na nchi mbalimbali duniani ikiwemo Ufaransa kujenga siku za baadaye
2024-05-07 14:34:15| cri

Marais wa China na Ufaransa wamekutana na wanahabari huko Paris baada ya kufanya mazungumzo.

Rais Xi Jinping wa China amesema, huu ni mwaka wa 75 tangu Jamhuri ya Watu wa China ianzishwe, baada ya juhudi kubwa za miaka 75, hali ya nchi na maisha ya watu yamebadilika kwa kiasi kikubwa, lakini kisichobadilika ni asili yetu ya amani na wema, moyo wa uvumilivu na ushirikishi na utafutaji wa haki na usawa. China inapenda kufanya juhudi pamoja na nchi mbalimbali duniani ikiwemo Ufaransa kuendeleza uhusiano wa ushirikiano wa kirafiki, kushikana mikono, kukabiliana kwa pamoja na changamoto, kujenga siku za baadaye juu ya msingi wa kuheshimiana.

Naye Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema, uhusiano kati ya Ufaransa na China una historia ndefu, nchi mbili zinaheshimiana na kuaminiana, anaona uhusiano huu utaweza kutoa mchango mkubwa zaidi nje ya uhusiano wa pande mbili, ukihimiza kwa kiasi kikubwa uhusiano kati ya Ulaya na China na utulivu wa dunia. Ametoa tena shukrani kwa rais Xi kufanya ziara yake ya tatu nchini Ufaransa, hasa katika wakati huu wa hali nyeti ya dunia, ziara hii ni muhimu sana.