Maonesho ya sanaa ya China ya “Kutoka Beijing hadi Paris-Safari ya Olimpiki ya Wasanii wa China na Ufaransa” yafunguliwa huko Paris
2024-05-07 10:33:24| cri

Wakati rais Xi Jinping wa China akifanya ziara nchini Ufaransa, Maonesho ya sanaa ya China ya “Kutoka Beijing hadi Paris-Safari ya Olimpiki ya Wasanii wa China na Ufaransa” yaliyoandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) na mashirika mengine ya Ufaransa yamefunguliwa mjini Paris.

Maonesho hayo yakitumia fursa ya maadhimisho ya miaka 60 tangu China na Ufaransa zianzishe uhusiano wa kibalozi na mwaka wa michezo ya Olimpiki ya Paris, yanasukuma mbele uenezi wa moyo na utamaduni wa Olimpiki kupitia kuunganisha miji miwili ya Olimpiki ya Beijing na Paris, ili kuhimiza China na Ufaransa kukutana, kuelewana na kuthaminiana.

Mkuu wa shirika la CMG Bw. Shen Haixiong, Waziri wa Utamaduni wa Ufaransa Bi. Rachida Dati na watu wengi mashuhuri kama 300 hivi kutoka sekta za uchumi, utamaduni, sanaa, michezo, elimu, vyombo vya habari na filamu wameshiriki kwenye ufunguzi wa maonesho hayo na kutembelea maonesho hayo.