Ethiopia yaingiza dola milioni 835 kutokana na mauzo ya kahawa ndani ya miezi 9
2024-05-08 08:51:14| CRI

Ethiopia imepata dola milioni 835 za Kimarekani katika kipindi cha miezi tisa iliyopita, kutokana na mauzo ya kahawa nje ya nchi.

Mamlaka ya Kahawa na Chai ya Ethiopia (ECTA) imesema Ethiopia ilisafirisha tani laki 1.74 za kahawa katika soko la kimataifa katika kipindi cha miezi tisa ya mwaka wa fedha wa Ethiopia 2023/24 ulioanza Julai 8. 

Naibu mkurugenzi mkuu wa ECTA Bw. Shafi Oumer, amesema mbali na wateja wa jadi ambao Saudi Arabia, Korea Kusini, Marekani, Ujerumani na Japan, katika miaka ya hivi karibuni Ethiopia pia imeweza kupata masoko mapya katika nchi nyingine ikiwa ni pamoja na China, Umoja wa Falme za Kiarabu na Sudan.

Katika mwaka uliopita wa fedha, Ethiopia ilipata dola bilioni 1.3 kutokana na mauzo ya nje ya tani 240,000 za kahawa.